MAAFISA WA POLISI 29 MBARONI UTURUKI

Takriban maafisa wa polisi 29 wanashtakiwa mjini Instabul Uturuki kwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi mnamo mwezi Julai.
Kesi hiyo ndio muhimu zaidi kuwahi kufanyika huku zaidi ya mashtaka 1000 yakiandaliwa. Huku maafisa wengine 40 wakizuiliwa kesi hiyo inatarajiwa kuwa kubwa zaidi katika historia ya Uturuki ya leo.
Washukiwa wanashtakiwa kwa kuwa na lengo la kuipindua serikali mbali na kujihusisha na kundi linaloongozwa na muhubiri anayeishi Marekani Fethullah Gulen, ambaye mamlaka inamlaumu kwa kupanga njama hiyo.

Comments