MAALIMU SEIF ATOA NENO ZITO KWA TUME YA UCHAGUZI
Katibu
Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema uamuzi wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC) wa kutaka pande zinazovutana ndani ya chama hicho
kuteua kwa pamoja jina la mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo
la Dimani kuwa ni wa kukurupuka.
Desemba
8, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima alisema fomu za
wagombea wa CUF katika uchaguzi huo zitapaswa kusainiwa na pande mbili
zilizo na mgogoro wa uongozi.
“Kipengele
cha 4 (5) (iii) cha Sheria ya Uchaguzi kinataka fomu za wagombea kwenye
chama chenye mgogoro zisainiwe na viongozi wakuu wote wawili kwa vile
wamethibitishwa na Msajili wa Vyama Siasa,” alinukuliwa Kailima.
Lakini
juzi, Maalim Seif alizungumzia uamuzi huo wa NEC na kusema kila chama
cha siasa kina kanuni na taratibu zake za kuwapata wagombea wa nafasi
mbalimbali.
“NEC
wamenishangaza kwa sababu nchi inaendeshwa kwa sheria na kanuni labda
nimuulize Kailima ameitazama Katiba ya CUF inasema nini kuhusu mchakato
wa wagombea? Tume inatoa uamuzi wa kisiasa ambao haukupaswa kutolewa na
chombo hiki muhimu,” alisema Maalim Seif.
Hata
hivyo, licha ya kushangazwa na hatua hiyo, Maalim Seif hakuwa tayari
kutoa msimamo wa CUF juu ya suala hilo akisema: “Ni mapema mno kusema
tutafanya nini?”
Tayari Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amesema lengo la NEC ni kutaka chama hicho kikose mgombea.
Wakati
Maalim Seif akieleza hayo, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa alisema:
“Tutaweka
utaratibu na watu wajitokeze ili tuweze kufanya uteuzi wa mgombea.
Ingawa kulikuwa na mgombea wa mwaka jana, nina imani watajitokeza
wengine na Baraza Kuu ndilo litamteua.”
Alisema
uchaguzi kwa ngazi udiwani hakuna tatizo kwa sababu mchakato wake
unaishia wilayani, lakini kwa ubunge lazima wakae pamoja.
CUF
imekuwa katika mgogoro baada ya Profesa Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti
mwaka jana kuibuka na kutaka kurejea kwenye nafasi hiyo, lakini viongozi
wengine wakamuwekea ngumu na kuibua mgogoro uliopo mahakamani.
Comments
Post a Comment