MABOMU YARINDIMA MBEYA MADEREVA BAJAJI WAFUNGA BARABARA KUU DAR-TUNDUMA-ZAMBIA

Mwandishi na Mtangazaji wa Kituo cha Redio Cha Big Star Cha Jijini Mbeya.

Madereva bajaji jijini Mbeya wamefunga barabara ya Dar-Tunduma-Zambia wakishinikiza wenzao 32 ambao wanashikiliwa na jeshi hilo tangu juzi wapewe dhamana.

Madereva hao wanashikiliwa na polisi kwa makosa matatu ikiwa ni pamoja na kuendesha bajaji bila leseni ya udereva, kufanya biashara ya bajaji bila kuwa na leseni ya biashara na kupita barabara kuu ambayo imepigwa marufuku kwa bajaji kuitumia.
Mwandishi wa habari wa kituo cha redio cha big star Dismass Mathias akizungumza na kipindi cha jaketi kutoka Kabwe ambapo madereva bajaji wameamua kuweka mawe barababarani na kukaa katikati ya barabara ili kushinikiza wenzapo kuachiwa.
Taarifa kutoka mahakamani inasema kuwa madereva hao watapewa dhamana Decemba 28 mwaka huu jambo linalopingwa na madereva hao kwa nguvu zote.
Taarifa zaidi itakujia kila kitakachojiri.

Comments