MADEREVA WAONYWA KUFUATA SHERIA



 Na Samwel Andrew, Dodoma
Maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yamefanyika mkoani hapa, katika viwanja vya mashujaa huku kitaifa yamekwisha fanyika mkoani Geita mwezi  Septemba mwaka huu.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana, akiwa ni mgeni rasmi, amesema kuwa kwa dereva yeyote atayeenda kinyume na utaratibu akamatwe na kufikishwa sehemu husika , na hata kufutiwa leseni ya utumiaji wa vyombo vya usafiri.
Rugimbana, ameongeza kwa kusema kuwa anawaomba wakuu wa wilaya washirikiane na mamlaka zote za barabarani kuweka alama zote stahiki za barabarani na kuiomba jamii iheshimu na kuzingatia alama hizo. 

Comments