MAGUFULI ATOA MADAWATI ZAIDI YA 800 CHATO

Wananchi wa Kata ya Buselesele katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita wamempongeza Rais John Pombe Magufuli kwa kutimiza ahadi yake ya kutoa madawati 850 ndani ya Wilaya hiyo hili kupunguza changamoto ya watoto kukaa chini.

Kituo kimoja cha luninga kimeshuhudia magari mawili makubwa yakishusha madawati hayo kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Buselesele yakitokea Mkoani Arusha yalikokuwa yakitengenezwa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mwalimu Eliasi Mataba amesema madawati hayo yatagawiwa kwenye mashule kulingana na mahitaji.

Comments