MAKALA ATAKA WALA RUSHWA WAFICHULIWE
![]() |
Mkuu Wa Mkoa Wa Mbeya Amos Gabriel Makala |
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amosi Gabriel Makalla amewataka wananchi
kusaidia katika kujenga maadili ya watumishi wa umma kwa kufichua vitendo vya
ukiukwaji wa wa utumishi wa umma ikiwemo rushwa.
Ameyasema
hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya maadili ambapo pia amewataka
watumishi wa umma kupiga vita rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu kwa
vitendo.
Ameongeza
kwa kusema kuwa serikali kwa kuzingatia maadili imetekeleza mipango mikakati
mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ya kupambana na rushwa ikiwa ni pamoja na
kuanzisha mkakati wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini Tanzania MKUKUTA na
kuanzisha siku ya maadili duniani ni ishara tosha ya kuonesha wamechukua hatua.
Aidha
amesema vita dhidi ya rushwa na madili ni ya kila mmoja sio kuziachia tu
mamlaka zinazohusika pekee kwa kuwa kwa kufanya hivyo ni ngumu kupambana na
rushwa na kuimaliza kabisa.
Naye
mkaguzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU wa kanda ya kusini
Joyce Shundi akitoa shukrani kwa mgeni rasmi amesema watafanyia kazi hotuba ya
mkuu wa mkoa kwa kutoa huduma yenye tija kwa jamii.
Amesema
wiki nzima hii ya maadili wametoa elimu kupitia vituo vya redio mkoani Mbeya,
kwenye shule, vyuo na taasisi za dini huku wakifanya usafi katika hospitali ya
Igawilo.
Maadhimisho
ya siku ya maadili kwa mkoa wa Mbeya yamefanyika katika viwanja vya ofisi ya
TAKUKURU mkoa wa Mbeya huku yakichagizwa na kauli mbiu inayosema kujenga na
kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi
ya rushwa.



Comments
Post a Comment