MALEKELA WA NIMR AWEKWA KIKAANGONI
Waziri wa
afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto,
Ummy Mwalimu, amemuita Mkurugenzi wa NIMR, Dk Mwele Malecela kutoa ufafanuzi
kuhusu taarifa ambazo amezitoa za kuwepo wagonjwa wa Zika nchini.
Waziri huyo amesema ugonjwa kama Zika unatakiwa
kutolewa taarifa na vyombo vya kimataifa baada ya kujadiliana kwa
kina na nchi husika badala ya kutolewa na taasisi moja pekee.
Jana taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa
NIMR ikitoa takwimu kuwa ilibaini kuwepo kwa wagonjwa 80 wa Zika
nchini, Wizara ya Afya imesema taarifa hizo hazijathibitishwa kimataifa .
Comments
Post a Comment