MARUFUKU KUWATANGAZA WANAOVUNJA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI KWENYE MITANDAO YA KIJAMII: KAMNDA MPINGA
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga |
Kamanda
wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema
wamesitisha kuwatangaza watuhumiwa katika mitandao ya kijamii baada ya
kupata malalamiko ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Hata
hivyo, amesema hadi wanasitisha walikuwa wamewakamata madereva 20 wa
Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuonyesha jamii ili wengine wenye tabia
hiyo wajifunze kupitia kwa wenzao na kuacha kuendesha wakiwa wamelewa.
“Kwa
sababu watu wengi wapo mtandaoni ilikuwa rahisi ujumbe kuwafikia kwa
wakati mmoja. Tulipata malalamiko ya haki za binadamu kuwa kufanya hivyo
kunawasababishia kudhalilika katika familia zao, tukaona tusitishe,”
amesema Mpinga.
Hata
hivyo, amesema pamoja na kusitisha utaratibu huo, madereva wasijisahau
kwa sababu vijana wapo kazini na wanaendelea kuwakamata wale wote
watakaokiuka sheria za barabarani, ikiwamo hiyo ya kuendesha wakiwa
wamelewa.
Awali,
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imelitaka Jeshi la Polisi,
Kikosi cha Usalama Barabarani, kuacha kuziweka hadharani picha za
madereva wanaotuhumiwa kukiuka sheria, badala yake liwafikishe
mahakamani kwanza.
Kauli
ya Tume hiyo imetokana na utaratibu ulioanzishwa na trafiki wa
kuwavisha mabango madereva wanaotuhumiwa kukiuka sheria ambayo
yameandikwa makosa yao na kurushwa kwenye mitandao ya kijamii kabla
hawajafikishwa mahakamani.
Mwenyekiti
wa Tume hiyo, Bahame Nyanduga amesema hayo wakati akifafanua kuhusu
kusitisha kuwaanika katika mitandao ya kijamii madereva wanaokamatwa na
trafiki kwa makosa ya usalama barabarani ikiwamo ulevi
Comments
Post a Comment