MCHINA MBARONI NA MASHINE 10

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei
Polisi mkoani Morogoro inamshikilia raia wa China, Guo You Yuan (48), mkazi wa Kibaoni mjini Ifakara wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, baada ya kukutwa na mashine 10 za kuchezesha bahati nasibu, zilizosambazwa katika mji huo, zinazodaiwa zipo chini ya kiwango.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alithibitisha jana kukamatwa kwa raia hiyo wa China baada ya kufanyika msako na wataalamu wa mamlaka ya bahati nasibu na kumkuta na mashine 10 zilizofungwa mjini Ifakara.

Hivyo alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa majira ya saa 4 asubuhi Desemba 13 mwaka huu, kufuatia msako ulioendeshwa na wataalamu wa bahati nasibu kutoka makao makuu Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine.

Kwa mujibu wa Kamanda Matei, wataalamu hao baada ya kuzikagua mashine hizo, walibaini ya kwamba hazikuwa na ubora unaotakiwa na pia zipo katika kiwango cha chini.

Comments