WAUGUZI WAREJEA KAZINI MADAKTARI WAENDELEZA MGOMO KENYA

Madaktari wa Kenya....
Wauguzi nchini Kenya wamesitisha mgomo wao baada ya chama chao kuafiakiana makubaliano ya kurejea kazini.

Wauguzi waliungana na madaktari kwenye mgomo wa nchi nzima tarehe 5 mwezi Disemba na kuathiri huduma katika hospitali za umma.
Madaktari wamekaidi maombi kadha ya kuwataka kurudi kazini wakisema kuwa watafanya tu hivyo wakati watalipwa mishahara walioafikiana na serikali mwaka 2013.
Wiki iliyopita serikali ilipeleka madaktari wa kijeshi kwenye hospitali kubwa zaidi nchini humo ya Kenyatta, baada ya madaktari wa mwisho 300 waliokuwa wakifanya kazi kujiunga na mgomo huo ambao umeathiri huduma za afya kote nchini.
Wagonjwa ambao walihitaji huduma za dharura walikosa huduma na kubakia wakiwa wamelala hospitalini.

Comments