MKURUGENZI JAMII FORUM MIKONONI MWA POLISI

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, kampuni inayomiliki mtandao maarufu, Jamii Forums,Maxence Melo anashikiliwa na polisi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media,Maxence Melo
Max ambaye ni mwanzilishi wa Jamii Forums, anashikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam (Central Police) na kwamba Jumatano hii atapandishwa kizimbani kwa madai kuwa amekataa amri ya jeshi la polisi kutoa taarifa za siri za watumiaji wa mtandao huo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye mtandao huo, Max amenyimwa dhamana.
“Maxence Melo anakamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari,” umeandika mtandao huo.

Comments