POTEZA MTOTO MWAKA MPYA UKIONE CHA MTEMA KUNI-RPC MTWARA
Wazazi na walezi mkoani Mtwara wametakiwa kuwachunga watoto wao katika
sherehe za sikukuu ya mwaka Mpya, na kwamba atakaepotelewa na mtoto kwa
uzembe atachukuliwa hatua za kisheria.
Wito huo umetolewa mkoani humo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara,
Thobias Sedoyeka na kuongeza kuwa jeshi hilo halitokuwa na huruma kwa
mzazi yeyote atakayetelekeza mtoto wake.
Jeshi hilo limeendelea kutoa tahadhari za kiusalama kwa watumiaji wa
vyombo vya moto kuhakikisha wanakuwa waangalifu na kuepuka kuendesha
vyombo vyao wakiwa wamelewa, pamoja na kuwataka wafanyabiashara wa
bar kuhakikisha wanafunga biashara zao katika muda uliopangwa.
Comments
Post a Comment