RAIS WA ISRAEL KUACHIWA HURU BAADA YA KUSHIKILIWA
Moshe Katsav |
Rais wa zamani wa Moshe Katsav anatarajiwa kuachiliwa huru baada ya kukaa miaka mitano jela kwa kosa la ubakaji.
Bodi
ya kutoa msamaha kwa wafungwa nchini Israel iliamua Jumapili kwamba
Katsav, 71, anaweza kuachiliwa huru wiki ijayo baada yake kukaa miaka
mitano jela.
Alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela.
Maombi yake mawili awali ya kutaka kuachiliwa huru mapema yalikuwa yamekataliwa.
Katsav alijizulu wadhifa wa urais mwaka 2007 baada ya kufunguliwa mashtaka ya ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia.
Amesisitiza mara kadha kwamba hana hatia.
Katsav alizaliwa nchini Iran na akaimbuka kuwa rais wa kwanza wa Israel aliyezaliwa katika taifa la Kiislamu.
Alichaguliwa mbunge wa chama cha Likud mwaka 1977 akiwa na miaka 30.
Comments
Post a Comment