SOMA HAPA KILICHOMUUA MENEJA WA DANGOTE
Meneja raslimali watu wa kampuni ya Dangote Industries Limited, Istifanus Bello |
Watu watatu wanaodaiwa kumteka na kumwua meneja raslimali watu wa
kampuni ya Dangote Industries Limited, Istifanus Bello, wamesema aliawa
kwa kutoa fedha ambayo haikutimia kama fidia kwa ajili ya kuachiliwa
watu waliokuwa wametekwa.
Watuhumiwa hao, Abdullahi Saliu, Babuga Adamu na Abubakar Gide, waliliambia gazeti la PUNCH Metro kwamba Bello aliwaudhi baada ya kuwapelekea Naira milioni 5.6 badala ya Naira milioni 10m zilizokuwa zimekubaliwa kwa ajili ya kuachiliwa kwa wataalam wanne wa kigeni wa kampuni hiyo waliokuwa wametekwa na kundi la watu hao.
Wanaotuhumiwa kumuua Istifanus Bello |
Kabla ya hapo, PUNCH Metro lilikuwa limeripoti kwamba Bello alikuwa amekwenda eneo la Ijebu-Igbo, Jimbo la Ogun, akiwa na Naira milioni 5.6 kama fidia ili kuwakomboa mateka hao.
Wakati wataalam hao wa kigeni waliachiliwa, yeye alikamatwa na kuuawa baadaye ambapo mwili wake uliripotiwa kupatwa na polisi katika mto mmoja.
Uchunguzi ulioendeshwa na Timu ya Kiitelijensia chini ya Inspekta
Jenerali wa Polisi Abba Kyari, ulisababisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao
– Saliu, Adamu na Gide — jijini Lagos, na katika majimbo ya Kwara na
Ogun.
Alhaji Aliko Dangote |
Watuhumiwa hao waliokuwa wafugaji wa kabila la Wafulani, Jumanne wiki hii walihamishwa kutoka makao makuu ya kikosi hicho jijini Abuja na kupelekwa katika kikosi maalum cha kupambana na wizi huko Ikeja, lagos, ili kusubiri upelelezi ukamilike.
Watuhumiwa hao waliokuwa
wanazungumza katika lugha ya Kiyoruba, walisema watu 10 wa kundi lao
ndiyo walioendesha oparesheni hiyo.
Saliu, mwenye umri wa miaka 20, mweneji wa Jimbo la Kano, alisema kundi
hilo lilikuwa linaongozwa na Alti ambaye alifyatua risasi iliyomuua
Bello.
PUNCH Metro liligundua pia kwamba watuhumiwa hao waliutupa mwili wa Bello katika mto na kuufungia gogo kubwa kuzuia usielee.
Kwa mujibu wa polisi, upelelezi kuhusu tukio hilo, bado unaendelea.
Comments
Post a Comment