SUGU APATA AJALI YA TATU NDANI YA MIAKA 3


December 17, 2016, imeripotiwa ajali ya gari kumuhusu Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la (SUGU), kwenye kivuko cha barabara (ZEBRA) na kumsababishia kifo mtoto ’15’ ambaye alifariki wakati akipelekwa hospitali.

Tukio hilo limetokea leo Desemba 17 majira ya saa mbili asubuhi huko katika eneo la Iyunga Jijini hapa, wakati gari ya Mbunge huyo ikiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege wa Songwe kwa ajili ya mapokezi ya kiongozi wa Kitaifa Freeman Mbowe.



AJALI YA PILI

January 10, 2015 ili ripotiwa kuwa Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amenusurika katika ajali ya gari eneo la Mlima Kitonga, wilaya ya kilolo mkoani Iringa.

Chanzo cha ajali hiyo kilitajwa kuwa ni kufeli kwa break hali iliyopelekea gari hilo kuanguka kichwa chini miguu juu wakati mbunge huyo akitokea Mbeya kuelekea Mikimi mkoani Morogoro kwenye mkutano wa hadhara.

Katika gari hilo aina ya Totoya Land Cruiser ambalo lilikuwa likiendeshwa na mheshimiwa Sugu, lilikuwa limebeba   watu wanne ambao wote walisalimika na kutoka salama licha ya michubuko ya mkononi aliyoipata mbunge huyo wa Mbeya Mjini.
AJALI YA TATU

Juni 19, 2013 Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi alipata ajali katika eneo la kasheki wilayani Hanan'g akielekea Arusha mjini.

Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu alikuwa akielekea Arusha mjini kuungana na wabunge wengine wa Chadema katika shughuli ya kuaga marehemu waliolipukiwa na bomu kwenye mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika ajali hiyo hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa, Mbunge huyo yuko salama, gari la Sugu limeharibiwa vibaya baada ya kugongana na basi la abiria.

Comments