UN NI SHIRIKA LA KUPIGA GUMZO BADALA YA KUFANYA KAZI- DONALD TRUMP
Kupitia akaunti
yake ya Twitter, amesema shirika hilo linamsikitisha kwa madai kwamba badala ya
kuwa shirika lenye hadhi kuu zaidi, limekuwa kama baraza la watu kukusanyika na
kupiga gumzo.
Hii ni baada ya
jaribio lake la kutaka kupinga azimio lililokemea mpango wa Israel kuendelea
kujenga makazi yao katika ardhi ya Wapalestina kufeli.
Baraza la usalama
la Umoja wa Mataifa limesema kuwa Israel inakiuka sheria za kimataifa kwa
kujenga katika ardhi ya Wapelestina.
Azimio hilo
lilipitishwa Ijumaa iliyopita huku Trump akitoa onyo kwamba mambo yatakuwa
tofauti wakati atakaposhika rasmi hatamu za uongozi wa Marekani.
Comments
Post a Comment