UN YAMTISHA YAHYA JAHMEH
Rais wa Gambia Yahya Jahmeh |
Rais wa Gambia Yahya Jammeh
atawekewa vikwazo vikali ikiwa atakataa kuondoka madarakani wakati
kipindi chake kitakapokamilika ifikapo tarehe 19 mwezi Januari, mjumbe
maalum wa Umoja wa Mataifa magharibi mwa Afrika ameonya.
Wakati wa mahojiano na shirika la Reuters, Mohammed Ibn Chambas alisema: "kuwa bwana Jammeh mwisho umefika na hawezi kuendelea kuwa rais chini ya misingi yoyote."
Tume ya uchaguzi nchini Gambia inasema kuwa mgombea wa upinzani Adama Barow alipata kura 222,708 au asilimia 43.3 ikilinganishwa na kura 208,487 au asilimia 39.6 alizopata Jammeh kenye uchaguzi wa Desemba mosi.
Mgombea wa tatu Mama Kandeh alipata kura 89,768 au asilimia 17.1.
Jammeh alitwaa madaraka nchini Gambia mwaka 1994 kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi na amelaumiwa kwa kuongoza moja ya tawala dhalimu zaidi barani Afrika.
Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa pia amekosoa hatua ya jeshi la Gambia ya kutwaa makao makuu ya tume ya uchaguzi kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Banjul.
Comments
Post a Comment