UNAIJUA SABABU ALIYO ISEMA WENGER BAADA YA KUFUGWA NA MAN CITY
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
amesema waamuzi nchini Uingereza wanalindwa kama simba kwenye kituo cha
kuhifadhi wanyama, baada ya Arsenal kulazwa na Manchester City 2-1
Jumapili.
Wenger anasema maamuzi mabaya ya refa yaliigharimu klabu yake ushindi.
Arsenal walikuwa mbele kabla ya Leroy Sane kusawazisha, ingawa kanda za video zinaonyesha alikuwa ameotea kidogo.
Na David Silva alikuwa pia amejenga kibanda ardhi ya City wakati Raheem Sterling alipofunga bao la ushindi.
Hata hivyo si wazi iwapo alingilia uchezaji wa kipa Petr Cech.
"Ni vigumu kukubali (matokeo) katika mchezo wa aina hiyo," amesema Wenger.
"Lakini,
inajulikana wazi, kwamba marefa wanalindwa sana kama simba kwenye kituo
cha kuhifadhi wa nyama, kwa hivyo inatulazimu kukubali uamuzi wao."
Alipotakiwa
kufafanua, Wenger alisema: "Nataka walindwe vyema, na nataka
wahakikishiwe usalama wao, lakini iwapo wangekuwa wanafanya maamuzi
sahihi, ingekuwa hata bora zaidi."
Aliongeza: "Ninaelewa kwamba
City wanaonekana kuwa an furaha sana - Hata mimi ningefurahi - lakini
nafikiri mabao hayo yalikuwa ya kuotea."
Gunners waliongoza ugenini Etihad kupitia bao la Theo Walcott mapema lakini City wakajikwamua kipindi cha pili.
Ushindi wao uliwawezesha kuwaruka Arsenal na kutua nambari ya pili kwenye jedwali, Arsenal nao wakashuka hadi nambari nne.
Wenger
pia alilaumu mwamuzi Arsenal waliposhindwa na Everton Jumanne, hatua
iliyomfanya meneja wa Everton Ronald Koeman kumcheka kwa kutilia shaka
uamuzi wa refa Mark Clattenburg.
Comments
Post a Comment