UPDATE: MAXENCE MELO NJE KWA DHAMANA

Mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence Melo, ambaye amekuwa akizuiliwa na maafisa wa polisi jijini Dar Es Salaam tangu Jumanne wiki iliyopita, amepewa dhamana na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Dar Es Salaam.
Bwana Melo alishtakiwa kwa makosa matatu Ijumaa.
Makosa hayo ni kuendesha na kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa nchini Tanzania, na kuzuia uchunguzi wa polisi kwa mujibu wa Sheria ya Makosa Kimtandao.
Hakuweza kuwasilisha ombi la kuachiliwa kwa dhamana Ijumaa na alizuiliwa gereza la Keko wikiendi.

Comments