WACHEZAJI 7 WA CAMEROOM WAGOMA KUITUMIKIA TAIFA LAO KWENYE AFCON 2017
Wachezaji saba wa taifa ya
Cameroon, wamesema hawataki kwenda kushiriki michuano ya kombe la
mataifa ya Afrika itayoanza kutimua vumbi kuanzia Januari 14 mwakani
huko nchini Gabon.
Nyota hao saba wasiotaka kuwa sehemu ya kikosi ni pamoja na beki mahiri wa Liverpool Joel Matip, ambae haijaichezea timu hiyo ya taifa toka mwaka 2014.
Kocha wa kikosi cha Cameroon Hugo Broos, amesema wachezaji wameweka maslahi yao binafsi juu ya yale ya timu ya taifa hivyo shirikisho la soka la nchi hiyo linatakiwa kuchukua hatua kwa wachezaji hao kwa mujibu wa kanuni za Fifa
Allan Nyom, anayechezea timu ya West Bromwich Albion, amemwambia kocha Broos, anataka kubaki kuendelea kuitumia klabu yake ili kulinda nafasi yake katika timu hiyo inayoshiriki ligi kuu England.
Wachezaji wengine wasiotaka kujuishwa kwenye timu hiyo ni Andre Onana wa Ajax Amsterdam, Guy N'dy Assembe wa Nancy, Maxime Poundje anayechezea Girondins Bordeaux ,Andre-Frank Zambo Anguissa wa Olympique Marseille pamoja na Ibrahim Amadou anayekipiga na Lille
Comments
Post a Comment