WAJUMBE KUTHIBITISHA MSHINDI WA URAIS WA MAREKANI LEO

Donald Trump
Wajumbe wa Jopo la Kumchagua Rais nchini Marekani wataanza utaratibu wa kuthibitisha matokeo ya uchaguzi wa urais nchini humo leo.
Katika uchaguzi wa awali, mshindi wa kura nyingi kawaida alikuwa ndiye anapata kura nyingi za wajumbe, na hatua ya kumuidhinisha ilikuwa tu ya kutimiza wajibu.
Lakini wakati huu, rais mteule Donald Trump wa chama cha Republican alishinda kwa kupata kura nyingi za wajumbe kutoka kwa majimbo yaliyokuwa yanashindaniwa.
Mpinzani Hillary Clinton, ambaye alikubali kushindwa, alipata kura nyingi za kawaida, ambapo alimzidi Bw Trump kwa zaidi ya kura milioni mbili unusu kote nchini humo.
Hilo limezua mjadala mpya kuhusu mchango wa Jopo la Kumchagua Rais ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama Electoral College nchini Marekani.
Watu karibu milioni tano wametia saini ombi la kuwataka wajumbe kuenda kinyume na utamaduni na kumpigia kura Bi Clinton.
Rais mpya ataapishwa mjini Washington tarehe 20 Januari.
Mara ya mwisho mgombea kushindwa kwa kura nyingi za kawaida lakini akakosa kuibuka mshindi wa uraia ni mwaka 2000 wakati Rais George Bush alishindwa na Al Gore kwa kura 500,000 lakini akafanikiwa kuingia ikulu.
Hillary Clinton
Tofauti ya kura za Clinton milioni 2.5 hata hivyo ni ya chini ikilinganishwa na kura milioni 3 za George W Bush alizomuacha nazo John Kerry mwaka 2004.
Uchaguzi wa mwaka 2004 ulikuwa na wapiga kura wengi zaidi kuliko wa mwaka 2016 kwa asilimia 1.7.
Ikiwa uchaguzi wa mwaka 2016 ulikuwa na asilimia kama hiyo basi watu milioni 2 zaidi wangehitajika kupiga kura.
Ikitokea kwamba kuwe na mgombea urais ambaye hajapata wingi wa kura za wajumbe (270), basi wabunge wa Bunge la Wawakilishi ndio huamua.
Kwa sasa bunge hilo lina wabunge 435. Chama chenye wabunge wengi, ambacho baada ya uchaguzi kufanyika ni Republican, bila shaka kitamchagua mgombea wake.
Makamu wa rais huchaguliwa na Seneti.
Hili limewahi kutokea wakati mmoja pekee, mwaka 1804, wagombea wanne walipogawana sana kura.
John Adams, aliyekuwa wa pili, alichaguliwa rais na Bunge badala ya Andrew Jackson aliyekuwa anaongoza kwa wingi wa kura.

Comments