WANANCHI NAO WAANZA KUTUMBUA MAJIBU



    Na Samwel Andrew, Dodoma
Wananchi wa Kata ya Ihumwa Manispa ya Dodoma, wamemkataa mwenyekiti wa mtaa wao Bwana William Njilimui, kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo za matumizi mabaya ya madaraka yake.
Wananchi wa mtaa huo wamebainisha sabababu za kumkataa mwenyekiti huyo kuwa ni pamoja na kutoitisha mikutano ya hadhara na kutosoma taarifa za mapato na matumizi kwa muda mrefu.
Wamesema kuwa kutumia madaraka vibaya imekuwa kati ya sababu za kumkataa mwenyekiti huyo bwana, njilimui, kwa kuwakamata wakazi wake ovyo na kuwatesa.
Sambamba na hayo wametaja sababu za kupotea fedha za miradi ya maji zilizizo tajwa kuwa jumla ya shilingi milioni nne, ambazo zimetokana na juhudi za wananchi wa mtaa wa Ihumwa.
Sanjari na hayo wananchi hao wamemchagua kiongozi wa muda ambaye ni Bi. Vickless  anaekaimu nafasi hiyo, huku wakisubiri uchaguzi ujao.

Comments