WANAOPATA STAREHE WANAPOKUWA MAKABURINI HAWA HAPA

Moja ya Nyumba Za Kifahari Mexico
Maishani, watu wengi hutaka kuishi katika nyumba nzuri na za kifahari. Wengi huwa hawafanikiwi. Lakini nchini Mexico, ambapo ulanguzi wa mihadarati umekithiri, wakuu wa magenge ya ulanguzi wa dawa za kulevya huishi maisha ya kifahari, na huendeleza hizi hata wanapokuwa wafu.

Nchini humo, utapata makaburi ambayo yangegeuzwa kuwa nyumba, matajiri wengi wangejivunia kuishi.
Ni makaburi makubwa yaliyojengwa na kuwekwa huduma za kisasa na vitu vingi vya anasa.
Kuna baadhi ya makaburi yenye viyoyozi vya kudhibiti viwnago vya joto na kuingiza hewa safi, kuna vioo visivyopenya risasi na baadhi yana hata vyumba ambavyo wageni wanaofika kutoa heshima kwa wafu, wanaweza kuketi na kupata kila kitu kinachopatikana katika nyumba za kifahari.
Baadhi yanakadiriwa kugharimu hadi £230,000 (Sh633 milioni za Tanzania; Sh29 milioni za Kenya)

Comments