WASANII MAREKANI WAMTOSA TRUMP

Rais Mteule wa Marekani Donald Trump
Ripoti zimeibuka kwamba Rais mteule wa Marekani Donald Trump amekosa wanamziki nyota ambao wangekutumbuiza sherehe yake ya kuapishwa hapo mwakani.

Wakati Rais anayeondoka Barack Obama alipokua anatawazwa wanamziki nyota Aretha Franklin na Beyonce waliwatumbuiza maelfu ya watu waliohudhuria kutawazwa kwake.Wakati wa Urais wake, Obama amewaalika kwenye ikulu wanamziki mashuhuri kama vile Rihanna, James Taylor, na Kendrick Lamar.
Inaonekana Rais mpya hana bahati ya kukumbatiwa na wanamziki. Kamati maalum inayotayarisha kuapishwa kwake imekua na wakati mgumu kuwatafuta wanamziki nyota ambao wataimba wakati wa sherehe hiyo ya Januari 20 mwaka ujao.
Baadhi ya duru zimesema wamakua wakiwasiliana na mameneja na maagenti wa wanamziki bila mafanikio yeyote. Mwamziki John Legend ambae amealikwa kwenye dhifa kadhaa wakati wa utawala wa Rais Obama amesema hajashangaa kutokana na hali ya sasa. '' Wasanii wote wanachukia dharau, sisi hutaka kuwa na maoni huru'', amesema Legend.
Ameongeza kusema,'' Tukimuona mtu anawagawanya raia na kuchochea chuki na dharau, sidhanii anaweza kuwavutia wasanii maana hawataki kuhusishwa na mtu kama huyu''.

Comments