Skip to main content
YAYA TOURE AKUBALI FAINI YA USALAMA BARABARANI
KOMBA
Baada ya kukutwa na kosa la kuendesha
gari akiwa amelewa kiungo wa Manchester City Yaya Toure amekubali kosa
hilo lakini amekiri kuwa hakutumia pombe kwa makusudi.
Nyota huyo mwenye miaka 33 alikamatwa
Desemba 3 huko Dagenham London baada ya kuzuiwa na maafisa wa polisi
wakati akiendesha gari na baada ya vipimo ilidaiwa kuwa Toure alikuwa
ametumia pombe.
“Kuendesha gari ukiwa umelewa ni kosa
kubwa na mimi nalifahamu hilo na sikutumia pombe makusudi, nalikubali
kosa na faini lakini napenda kuomba msamaha kwa hili. Napenda pia
kuwashukuru familia yangu, uongozi na wafanyakazi wote wa Manchester
City, wanasheria wangu na mashabiki kwa msaada wao walionipa katika
wakati huu mgumu. ” Amesema Toure kupitia taarifa aliyotoa leo.
Comments
Post a Comment