KOMBA
Wengi wanaimba muziki lakini
kuna watu ukiwasikiliza mistari yao unaweza ukajiuliza mara mbili hivi
ni kweli yeye anaweza kuimba kile anachoimba ? Ama mistari atakuwa
ameandikiwa ? Lakini ukweli wa mambo huwa wengi wanaandika wenyewe. Mtu
kama Fid Q kwa mistari yake anayoandika inaendana na umri wake hivyo
hakuna shida ya kumuongelea yeye sana.
KOMBA
Huyu dogo nashindwa kuelewa
kama mistari anayoandika kweli yake au ameandikiwa baadae nakuja
kugundua kuwa mistari yake na ameandika mwenyewe. Sasa najiuliza tena
kuna chochote huwa anawaza wakati wa kuandika mistari ? Hapo sasa sipati
jibu ila huu ndio usanii wenyewe. Kila mmoja ana njia zake anazopita
kuikabili biashara hii.
Killer ameweza kuandika
mistari katika ngoma zake ambazo zinaeleweka na kuufanya muziki uzidi
kuwa mtamu hasa kwa ugumu wa mashairi yake. Hebu pitia nyimbo ya Miss
Super star aliyoimba na Bright pamoja na Nemo alivyojaribu kuchambua mle
ndani ya wimbo huu hiyo ni mifano midogo tu jaribu kupitia nyimbo
aliyoimba na Banana Zorro sikiliza vizuri humo. Tatizo letu hatupitii
kusikiliza mashairi bali tunasililiza ngoma kali pekee ambapo hata
mashairi yakiwa poa nyimbo hizo inabuma. Lakini usisahau ngoma iliyomtoa
aloyomshirikisha Belle 9 Dear Gambe.
Hii ni hazina kubwa miongoni
mwa wasanii wetu Tanzania ambao kama tusipowapuuza wataandika ngoma
zitasikilizwa hadi vitukuu vyetu kwa mashairi mazuri.
Comments
Post a Comment