ZAIDI YA MILIONI 526 KUTENGENEZA BARABARA SONGEA

Soko Kuu Songea


Na Mwandishi Wetu, Songea
Halmashauri ya Manispaa ya Songea ina mtandao wa barabara wenye jumla ya km 336.47 zinazohudumiwa na Halmashauri.

Kati ya hizo, km 14.76 ni za lami, km 119.21 ni za changarawe na Km 202.50 ni za udongo.

Katika mwaka wa fedha 2015/2016, Halmashauri ya Manispaa ya Songea iliidhinishiwa kutumia jumla ya Tsh. 526,120,000.00 kwa ajili ya matengenezo ya barabara kutoka mfuko wa barabara.

Fedha hizi zilikusudiwa kugharamia matengenezo ya barabara

Km.134.1.

Hadi kufikia Juni 2016 Halmashauri ya Manispaa ya Songea ilikuwa imepokea jumla ya Tsh.736,235,673 toka Mfuko wa barabara.

Kati ya fedha hizo Tshs .179,834,930.85 ni za mwaka wa fedha 2015/2016 na zilizosalia ni bakaa toka mwaka wa fedha 2014/2015.

Katika kipindi cha Julai hadi Oktoba 2016 Halmashauri ya Manispaa imetumia jumla ya Tshs 218,309,463 ikiwa ni bakaa ya mwaka 2015/2016 kwa ajili ya kufanyia matengenezo ya barabara zake.

Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa mwaka wa fedha 2016/2017 imetenga jumla ya Tshs 1,527,510,000 kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara (Road Fund).

Kupitia mfuko wa barabara,Halmashauri inatarajia kufanya matengenezo ya jumla ya km 215.10, na ukarabati wa madaraja 6 kama ifuatavyo:

Matengenezo ya kawaida mara mara (Routine maintenance) km 175.35 Tshs 383,080,000 na Matengenezo ya maeneo korofi (Spot improvement) km 21.15 Tshs 153,230,000.

Matengenezo ya muda maalum (Periodic maintenance) km 18.60 Tshs Tshs 609,230,000, ujenzi na ukarabati wa madaraja 6 Tshs 304,470,000.00 na usimamizi na ufuatiliaji Tsh.77,500,000.

Hata hivyo hadi kufikia Oktoba 2016 Halmashauri haijapokea fedha hizo kwa ajili ya matengenezo ya barabara.

Katika mwaka wa fedha 2015/2016 Halmashauri ilitengewa jumla ya Tsh.546,000,000 toka bajeti ya maendeleo kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi barabara ya Songea girls – Mateka Km 1 kwa kiwango cha mawe kazi hii imetangazwa.

Fedha iliyokwisha pokelewa hadi Oktoba 2016 ni Tsh.224,000,000.00

Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa Mwaka wa fedha 2015/2016 iliidhinishiwa kutumia jumla ya Tshs 7,544,528,271.28 kwa ajili ya kutekeleza program ya uboreshaji wa Miji na Manispaa (ULGSP).

Kati ya fedha hizo Tshs 377,226,413.56 ni kwa ajili ya kujenga uwezo na Tshs 7,167,301,857.71 ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu.

Fedha zote Tshs 7,544,528,271.28 zilizoidhinishwa kwa ajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali zilizomo kwenye miradi ya ULGSP

zimepokelewa.

Awamu ya kwanza Mei 2016 zilipokelewa Tshs 2,724,578,927.56 na awamu ya pili Oktoba 2016 zilipokelewa Tshs 4,819,949,343.7.

TAARIFA HII IMETOLEWA NA

ALBANO MIDELO

AFISA HABARI WA MANISPAA YA SONGEA

Comments