ZSA ZSA GABOR AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 99
Mwigizaji maarufu Zsa Zsa Gabor amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 99.
Mumewe
wa sasa Frederic von Anhalt amesema mwigizaji huyo alifariki baada ya
kupatwa na mshtuko wa moyo akiwa amezingirwa na marafiki na jamaa.
"Kila mtu alikuwa hapo. Hakufariki akiwa peke yake,"
Alitengeneza zaidi ya filamu sita lakini alijulikana zaidi kwa kuwa na wanaume wengi na kupenda almasi.
Kwa
hesabu zake mwenyewe Zsa Zsa Gabor aliwahi kuolewa mara nane na nusu,
hakuchukulia ndoa yake kwa Mhispania mwaka 1983 kuwa ndoa kamili.
Alikuwa maarufu kwa miongo kadhaa, kabla ya hata kuibuka kwa Paris Hilton au Kim Kardashian.
Sauti yake ya kuburudisha ilikuwa pia historia.
Akitoa
maoni juu ya kushindwa kudumu katika ndoa Gabor alisema katika ndoa zake
alifanywa kama msimamizi wa nyumba kwa sababu kila alipokuwa akipewa
talaka yeye aliachiwa nyumba.
Zsa Zsa Gabor alizaliwa mjini
Budapest nchini Hungary tarehe 6 Februari 1917 na akahamia Marekani
wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Aliigiza filamu yake ya kwanza Hollywood mwaka 1952.
Aliigiza zaidi ya filamu 70, lakini alifahamika sana kwa maisha yake ya kifahari.
Aliolewa
mara ya kwanza akiwa na miaka 20 na ndoa yake iliyodumu muda mrefu
zaidi ilikuwa yake ya mwisho alipokuwa na miaka 70 kwa Frederic von
Anhalt.
Gabor alitawazwa Miss Hungary mwaka 1936, lakini baadaye
akapokonywa taji hilo kwa kuhadaa kuhusu umri wake ndipo aruhusiwe
kushiriki shindano hilo.
Aliigiza karika filamu maarufu kama vile
Moulin Rouge (1952), Lili (1953) na Queen of Outer Space (1958). Hivi
karibuni, aliigiza katika filamu ya Nightmare kwenye mwendelezo wa
filamu za Elm Street na pia kwenye filamu za ucheshi za Naked Gun.
Comments
Post a Comment