30 WAHOFIWA KUPOTEZA MAISHA HOTELINI NCHINI ITALIA

Waokoaji wanasema kuwa hadi watu 30 wametoweka baada ya hoteli moja katikati mwa Italy kuangukiwa na maporomoko ya theluji yaliosababishwa na tetemeko la ardhi.
Waokoaji walifanya juhudi za usiku kucha kufika katika hoteli ya Rigopiano, huku wa kwanza akifika kwa kutumia ubao wa kutelezea juu ya theluji.
Barafu iliosombwa na theluji hiyo ilifunga barabara za kuingia katika eneo hilo.
Mtu mmoja amepatikana amefariki katika barafu hiyo. Wawili wamepatikana wakiwa hai lakini wengine wengi bado wamefukiwa chini ya theluji hiyo.
Afisa mmoja amesema kuwa kuna watu wengi waliofariki katika hoteli hiyo.
 Eneo la milima katikati mwa Italy lilikabiliwa na msururu wa mitetemeko ya ardhi siku ya Jumatano pamoja na mitetemeko mingine usiku kucha.
Mitetemeko hiyo ya ardhi imesababisha maafa mengi kutokana na kimbunga cha hivi majuzi ambacho kiliangusha miti ya stima mbali na kufunga barabara zinazoelekea vijijini.
Operesheni za uokoaji zinaendelea katika maeneo mengine ya jimbo hilo.

Comments