40 WANUSURIKA KIFO AJALINI MTWARA MAJERUHI WAKIMBIZWA HOSPITALI

Zaidi ya watu 40 waliokuwa wakisafiri na Lori lenye namba za usajili T294 BRZ kutoka Masasi Mkoani Mtwara kwenda Mnero wilayani Nachingwea mkoani Lindi kwa ajili ya mnada wa bidhaa mbalimbali wamenusurika kufa baada ya Lori hilo kupinduka katika kijiji cha Nammanga Nachingwea.

Majeruhi kadhaa wa ajali hiyo walikimbizwa katika hospitali ya Ndanda na Hospitali ya wilaya ya Nachingwea.

Mwandishi wa blog hii amefika katika eneo la ajali katika Kijiji cha Namanga na kushuhudia Gari hilo linalomilikiwa na chama cha msingi na ushirika Namijati wilayani Masasi likiwa limepinduka huku majeruhi wakiwa wamekimbizwa hospitali kwa matibabu

Mmoja kati ya Shuhuda wa tukio hilo na baadhi ya abiria ambao ni wafanyabiashata waliokuwa ndani ya gari wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi.

Comments