ADAMA BARROW SASA KUAPISHWA NCHINI SENEGAL

Adama Barrow
Rais wa Gambia Yahya Jammeh amekataa kuondoka madarakani kutoa nafasi ya kuapishwa kwa Adama Barrow hata baada ya makataa aliyopewa na Senegal kumalizika.
Barrow alipangiwa kuapishwa kuwa rais mpya Alhamisi, na wanajeshi wa nchi za Afrika Magharibi wako tayari kuingilia kati.
Rais huyo mteule sasa ametangaza kwamba ataapishwa katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal mwendo wa saa 16:00 GMT (saa moja Afrika Mashariki).
Ametangaza hayo kupitia mtandao wa Twitter na kuwaalika wananchi kuhudhuria.
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz alikutana na Bw Jammeh kwa mazungumzo ya dakika za mwisho kabla ya kuondoka na kwenda Senegal kwa mazungumzo na rais Macky Sall.
Bw Barrow alitangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu mwezi uliopita na Bw Jammeh mwanzoni alikubali kushindwa lakini baadaye akapinga matokeo hayo.
Pendekezo la wanajeshi wa mataifa ya Afrika Magharibi kuingilia kati kumuondoa madarakani linaungwa mkono na Nigeria na nchi nyingine za kanda hiyo.
Mkuu wa majeshi ya Gambia Ousman Badjie amesema wanajeshi wake hawatapigana na wanajeshi wa Senegal iwapo wanajeshi hao wataingia nchini Gambia, shirika la habari la AFP limeripoti.
Bw Jammeh ametawala Gambia tangu alipochukua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1994.
Jumatano ilifaa kuwa siku yake ya mwisho madarakani lakini Bunge la nchi hiyo lilipitisha azimio la kumruhusu kuendelea kuongoza kwa miezi mingine mitat

Comments