AJALI YA NDEGE YAUA WATU 35
Watu
zaidi ya 32 wamefariki baada ya ndege ya kubeba mizigo ya Uturuki,
iliyokuwa safarini kutoka Hong Kong kuangukia nyumba za watu karibu na
mji wa Bishkek nchini Kyrgyzstan.
Taarifa zinasema wengi wa waliokufa ni watu waliokuwa ardhini, ndege hiyo aina ya Boeing 747 ilianguka karibu na uwanja wa ndege wa Manas, takriban kilomita 25 kutoka mji mkuu Bishkek,
Nyumba
zaidi ya 15 zimeharibiwa na watoto kadha wanaripotiwa kuwa miongoni mwa
waliofariki. Imeelezwa kuwa hali ya hewa ilikuwa mbaya na kulikuwa na
ukungu, ingawa chanzo hasa cha ajali hiyo hakijathibitishwa.
Kuna
taarifa zinasema kuwa kwenye ndege hiyo kulikuwa na wahudumu wanne na
mhudumu mmoja wa ndege amenusurika, watu kadhaa wamepelekwa hospitalini
wakiwa na majeraha.
Msemaji
wa huduma za dharura nchini humo Muhammed Svarov, ameambia AFP kwamba
huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka na juhudi za kuwasaka
walionusurika zinaendelea.
Comments
Post a Comment