AMUUA MKEWE KISA WIVU WA MAPENZI
Mwanamke
mmoja mkazi wa Mikumi wilayani Kyela, Mbeya aliyefahamika kwa jina la
HILDA SIGARA amefariki dunia akiwa anapelekwa Hospitali kwa matibabu
baada ya kupigwa nyundo kichwani na mume wake aitwaye REBSON TWEVE umri
kati ya miaka 30 – 35
Kamanda
wa polisi mkoani humo DCP Dhahiri Kidavashari amesema tukio hilo
limetokea mnamo tarehe 05.01.2017 majira ya saa 12:00 asubuhi ambapo
imedaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi kwani
inasadikiwa mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa ana mahusiano ya
kimapenzi na mwanaume mwingine.
Amesema
katika eneo la tukio kumekutwa nyundo moja, kisu kimoja na fimbo ya
muanzi ambavyo vinasadikiwa kutumika katika tukio hilo.
Mwili
wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya Kyela ukisubiri kufanyiwa
uchunguzi wa kitabibu na upelelezi unaendelea huku mtuhumiwa akiwa
ametoroka mara baada ya tukio na juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Aidha,
katika matukio mengine kamanda huyo amesema kuwa jeshi la polisi
limepokea taarifa za kujinyonga kwa watu wawili ambao miili yao imekutwa
ndani ya nyumba zao katika maeneo tofauti.
Watu
hao ni pamoja EDWARD PETER mfanyabiashara na Mkazi wa Majengo na
aliyekutwa amekufa chumbani kwake huku mwili wake ukiwa hauna majeraha
yoyote, na mwingine ni ROBERT MWAISENYE Mkazi wa Mbugani wilayani Chunya
ambaye alikuwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya manila akiwa ndani ya
nyumba yake.
Comments
Post a Comment