ARSENAL YAWAONGEZEA MKATABA HAWA HAPA
Wachezaji wa Arsenal Olivier Giroud, Laurent Koscielny na Francis Coquelin wameongeza kandarasi zao na klabu hiyo.
Arsenal
haijatangaza kuhusu kiwango cha kandarasi hizo ,lakini Koscielny
amesema katika mtandao wa Twitter kwamba ataongeza kandarasi yake hadi
mwaka 2020.
''Tunafurahi kwamba wachezaji watatu muhimu wameamua
kusalia nasi kwa kipindi cha muda mrefu'', Mkufunzi wa Arsenal Arsene
Wenger amenukuliwa akisema.
Wachezaji hao wa Ufaransa wamekuwa
wakishiriki kila mechi huku Giroud akiweka kandarasi hiyo baada ya
kufunga mabao manne katika mechi nne likiwemo bao lake la 'nge' dhidi ya
Crystal palace.
''Francis ameimarika pakubwa katika kipindi cha miaka michache iliopita kwa sababu ana maono kila siku'', alisema Wenger.
''Olivier
ana uzoefu katika mechi kubwa na ameimarika zaidi tangu ujio wake
hapa. Koscielny ni kiungo muhimu wa kikosi chetu na ninaamini ni
mmojawapo wa mabeki wazuri duniani''.
Comments
Post a Comment