CHELSEA KUKATA RUFAA KADI NYEKUNDU YA JOHN TERRY
Meneja wa Chelsea Antonio Conte
amesema klabu hiyo inatafakari uwezekano wa kukata rufaa dhidi ya kadi
nyekundu aliyoonyeshwa nahodha
John Terry wakati wa mechi ya FA
Jumapili.
Chelsea walilaza Peterborough 4-1 mechi hiyo.
Blues
walipokuwa mbele 3-0, Terry, 36, alimwangusha mshambuliaji Lee Angol na
refa Kevin Friend akaamua kuwa alikuwa mchezaji wa mwisho wa Chelsea.
"Lazima uheshimu uamuzi, lakini wakati huu labda tutakata rufaa," alisema Conte.
Mechi hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Terry kuwa kwenye kikosi cha kuanza mechi tangu Oktoba.
Chelsea
wakishindwa kwenye rufaa hiyo, basi Terry hatakubaliwa kucheza mechi ya
Ligi ya Premia ugenini kwa mabingwa watetezi Leicester City tarehe 14
Januari.
John Terry ameoneshwa kadi tatu kati ya sita nyekundu walizoonyeshwa wachezaji wa Chelsea karibuni zaidi
Comments
Post a Comment