DEMOCRATIC WAGOMA KUHUDHURIA HAFLA YA KUAPISHWA KWA RAIS MTEULE WA MAREKANI DONALD TRUMP
Wabunge kadhaa wa kiume na wa kike
wa chama cha Democratic nchini Marekani wamesema kuwa hawataudhuria
sherehe za kuapishwa kwa Rais Donald Trump, Ijumaa hii.
Hii ni
baada ya Trump kumkosoa John Lewis, mbunge na mtetezi maarufu, mwenye
sifa tele wa haki za binadamu, baada ya kuhoji uhalali wa ushindi wa
Donald Trump.
Mtoa maoni mmoja wa siasa za msimamo mkali Bill Kristol, amesema kuwa Bwana Trump anampa Rais wa Urusi heshima kubwa mno.
John
Lewis ni mmoja wa maspika ambaye bado angali hai kati ya waandamanaji
wa kutetea haki za binadamu, waliohudhuria mkutano uliofanyika mwaka
1963 mjini Washington, na kuhutubiwa na Martin Luther King.
Amesema kuwa hatohudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Trump siku ya
Ijumaa, kwa sababu hamtambui kama Rais aliyechaguliwa kwa haki kutawala
Marekani.
Kumjibu, Bwana Trump alisema kuwa hayo yote anayosema
Bwana Lewis, ni maneno matupu yasio na matendo, huku akimshauri
kushughulikia maslahi ya watu wa Wilaya yake ya Georgia.
Comments
Post a Comment