JAHAZI LAUA 12 HUKO TANGA
Jahazi
hilo lenye namba za usajili Z5512 MV Burudani maarufu kama Sayari
lilikuwa likitokea eneo la Bandari Bubu ya Sahare kuelekea Visiwani
Pemba ambapo lilipofika eneo la Jambe, chombo hicho kilipigwa na dhoruba
kali na hivyo kumshinda nahodha wake Badru Saidi na kuzama
Akizungumza
na Mtandao huu,Mbunge Mussa alisema amepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa za ajali hiyo na kuwataka ndugu na jamaa kuwa na uvumilifu na
kuhaidi kuwa nao bega kwa bega.
Licha
ya hivyo lakini pia mbunge huyo alikabidhi sanda 12 kwa ajili ya maziko
ambayo yanafanyika leo na kesho kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.
Ajali
hiyo ambayo ilitokea usiku wa kuamia leo kwenye eneo la kisiwa cha
Jambe kandokando ya bandari ya Tanga imeacha simamanzi kubwa kwa wakazi
wa mji huu na viunga vyake.
Alisema
kuwa yeye kama mbunge wa Jimbo la Tanga yupo nao bega kwa bega na
kuwaombea mwenyezi mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.
“Ajali
sio jambo ambalo tunalipanga bali ni mipango ya mwenyezi mungu lakini
pia nivitake vyombo vya usafiri majini kuhakikisha havipakii mizigo
mingi zaidi ya uwezo wao kwani hali hiyo inaweza kusababisha ajali
“Alisema.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba alithibitisha kutokea tukio
hilo na kueleza hivi sasa vyombo vya ulinzi na usalama wapo kwenye
mchakato wa kutafuta watu wengine kwenye bahari ya hindi.
Alisema kati ya miili hiyo iliyopatikana mpaka sasa wanaume watano na wanawake 7 wameweza kuokolewa katika tukio hilo.
Aidha
alisema mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana hivyo
wanashirikiana na vyombo vyengine ili kubaini ingawa kwa mujibu wa
mashuhuda chanzo chake kinatokana na chombo hicho kupigwa na wimbi eneo
la nyuma na kukosa mwelekeo na kuzama baharini.
Kwa
upande wake,Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo,Dkt
Goodluck Mbwilo alithibitisha kupokea maiti 12 pamoja na majeruhi 25.
Alisema
kati ya majeruhi hao 18 ni watu wazima huku watoto wadogo wakiwa ni
saba ambao waliweza kupewa huduma ya kwanza na kuendelea na matibabu
mengine.
Comments
Post a Comment