KIJANA MDOGO AMPIGA KOFI WAZIRI MKUU WA ZAMANI
Manuel Valls |
Waziri mkuu mstaafu wa Ufaransa
Manuel Valls amekashifiwa alipokuwa akihamasisha katika kampeni za
chama cha kisoshalisti katika uchaguzi mkuu wa kiti cha Urais nchini
Ufaransa.
Alipokuwa akihutubia katika ukanda wa Magharibi mwa mji
wa Brittany alipigwa kofi na kijana mdogo alipokuwa akisalimia kwa
kushikana mikono.
Mlinzi binafsi wa Bwana Valls alimkamata kijana huyo kooni kisha akamtupa chini.
Manuel Valls hajajeruhiwa katika tukio hili.
Comments
Post a Comment