KIJANA MWEUSI ASABABISHA BINTI WA KIZUNGU KUTENGWA NA WAZAZI WAKE
Mwanafunzi mmoja amechangisha zaidi
ya dola 10,000 kupitia mchango wa raia baada ya kudai kwamba mamake na
baba walikata uhusiano wake naye kwa kuwa na mpenzi mweusi.
Allie Dowdle anasema wazazi wake walikataa kumpatia fedha kwa sababu hawakupenda uhusiano wake na kijana huyo mweusi.
Akiandika katika ukurasa wake wa GoFundMe ,Allie alisema: Nikiwa na
umri wa miaka 18 wazazi wangu wamekataa kunifadhili katika maisha yangu
ya baadaye ,na kunipokonya raslimali zangu zote.
Babake msichana huyo hatahivyo amekana kwamba sababu ya kukata uhusiano huo ni ile ya ubaguzi wa rangi.
Allie anasema kuwa yeye na Michael Swift wamekuwa katika husiano wa
kimapenzi kwa takriban mwaka mmoja baada ya kuwaelezea wazazi wake
lakini swala hilo likazuka tena baada ya Michael kukutana na wazazi wake
msichana huyo.
Anadai kwamba baada ya mkutano huo wazazi wake
walimtenga na sasa hawezi kupata fedha alizohifadhiwa ,gari, simu na
hawezi kulipia masomo yake.
''Babangu hakunipa sababu nyengine, aliniambia kwamba siruhusiwi
kumuona Michael tena'' ,alisema. Kwa nini? kwa sababu ya rangi ya ngozi
yake.
''Sitasahau vile wazazi wangu walivyonikaripia walipoelezea
vile walivyokasirishwa nami kwamba ningeweza kutafuta mtu mwengine
mzuri zaidi''.
Comments
Post a Comment