LIPUMBA AKOMBA MAMILIONI YA SERIKALI HALI YA MBAYA ZAIDI

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimedai kuibiwa fedha za ruzuku zaidi ya Sh milioni 369 huku chama hicho kikiwahusisha waliokuwa viongozi wa chama hicho, akiwemo Mwenyekiti wao,
Profesa Ibrahim Lipumba na Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya.

Aidha chama hicho kimemuomba Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Gavana wa Benki Kuu (BoT), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Ofisi ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na vyombo vingine vinavyohusika, kuchukua hatua za dharura za kuokoa fedha hizo.

Hata hivyo, Sakaya ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF upande wa Bara, alisema fedha hizo hazijaibiwa kama ambavyo inadaiwa, isipokuwa kwa nafasi aliyonayo ndani ya chama alimuandikia Msajili kuomba fedha hizo kwa ajili ya chama kuingia katika uchaguzi, ndipo zikaingizwa katika akaunti hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saalam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, Julius Mtatiro alisema CUF imeibiwa Sh 369,378,502.64 za ruzuku.


Hata hivyo, Mtatiro alisema kuwa baada ya kugundua utoroshwaji huo, CUF imejiridhisha kuwa akaunti ambayo Hazina wameshiriki kuitumia kutorosha fedha za umma na mali ya CUF ni akaunti ya CUF, ambayo hutumiwa na Wilaya ya Temeke kwa ajili ya kupokea mgawo wa ruzuku kutoka kwa Chama Taifa.

Aidha, Mtatiro alisema vikao vya kitaifa vya CUF, yaani Kamati ya Utendaji ya Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa, havikuwahi kupitisha maamuzi yoyote kwamba fedha za CUF ziwekwe katika akaunti hiyo ya wilaya iliyoko NMB Temeke.



Alisema kesho yake, wakiongozwa na Malima walikwenda katika Benki ya NMB tawi la Temeke na wakatoa Sh milioni 69 na kuhamisha Sh milioni 300 kwenda kwenye akaunti ya mtu binafsi kwenye akaunti ya NMB 41401600207 ikimilikiwa na Diwani wa CUF wa Handeni mkoani Tanga.

“Mtu huyu ni wa karibu na Lipumba na ni mmoja kati ya wanachama wanane waliosimamishwa uanachama na Baraza Kuu, jana (juzi) akaunti hii ilikuwa kwenye mchakato wa kuondoa fedha hizo kutoka kwenye akaunti hiyo, na kubaki na Sh 207,907 tu,” alisema Mtatiro.

Alisema mtu huyo alitoa Sh milioni 100 kutokea Benki ya NMB tawi la Magomeni, kisha akiwa hapo Magomeni akatoa Sh milioni 50, tawi la Kariakoo alitoa Sh milioni 100 na mwisho akatoa tena Sh milioni 49.5 huku wakiwa na ulinzi wa polisi na gari ya chama hicho akiwa na Sakaya na wengine.

“Hadi tuongeavyo sasa miezi mitano CUF inadai ruzuku ya Shilingi milioni 635 na kwa kuwa fedha zilizotoroshwa Hazina zimepelekwa kwenye akaunti isiyotambuliwa Bodi ya Wadhamini ya chama inatamka kuwa hadi sasa ruzuku yake ni Shilingi 635,000,000,” alisema Mtatiro.





A

Comments