MAPYA YAIBUKA GAMBIA, MAKAMU WA RAIS NAYE AJIUZULU
Makamu wa rais nchini Gambia Isatou
Njie-Saidy amejiuzulu saa chache kabla ya muda wake wa kuongoza kutimia
,AFP imenukuu duru za familia yake.
Waziri wa mazingiura na elimu
ya juu pia alijiuzulu,ikiwa ni msururu wa mawazuri kumtoroka bw Jammeh
kufuatia hatua yake ya kukataa kujiuzulu baada ya zaidi ya miongo
miwili afisini AfP imeripoti.Wakati huohuo wakili wa rais Yahya Jammeh ametorokea nchini Senegal baada ya kumuandikia barua rais Jammeh akimtaka kuachilia mamlaka gazeti la Nigeria Primium times limesema.
Edu Gomez alisema kuwa amemfanyia kazi Jammeh chini ya shinikizo chungu nzima
Gazeti hilo pia limenukuu barua hiyo ikisema: Siku ya Jumanne tarehe 17 mwezi Januari 2017, mwanangu na mimi tulifanya uamuzi muhimu kutafuta hifadhi katika taifa jirani la Senegal.Hatua hii tuliona ni muhimu kutokana hofu inayoendelea kutanda na wasiwasi kila wakati.
Bw Gomez alimwakilisha Jammeh katika harakati za kufutilia mbali ushindi wa kiongozi wa upinzani Adama Barrow katika uchaguzi wa tarehe mosi Disemba.
Comments
Post a Comment