MAZOMBI YAVAMIA OFISI ZA CUF YAPORA, YAJERUHI, YATEKA

Watu wasiojulikana maarufu kama mazombi wameivamia ofisi ya Chama cha Wananchi (CUF) katika Jimbo la Dimani Wilaya ya Magharibi B. 
Katika tukio hilo lililotokea saa 6.30 usiku wa kuamkia jana, inadaiwa mazombi hayo yalipora mali, kujeruhi watu na kuwateka wengine wa nyumba jirani na ofisi hiyo. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo huku CUF wakitaka uchunguzi uanze mara moja kuwabaini wahalifu.

Comments