MBOWE KAZUNGUMZA HAYA BAADA YA KUKAMATWA KWA EDWARD LOWASSA

Freeman Mbowe


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amesema kuwa kitendo cha kumkamata Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa mkoani Geita kimedhihirisha polisi kutumika na Chama Cha Mapinduzi wakati wa chaguzi mbalimbali.
Mbowe ametoa kauli wakati akifungua Kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichohudhuriwa na wajumbe mbalimbali akiwemo Lowassa pamoja na baadhi ya wabunge.
Mwenyekiti huyo amesema jeshi la polisi limekuwa likiwakamata na kuwaweka ndani viongozi mbalimbali wa chama chake kwa shinikizo la chama cha mapinduzi CCM na kuwataka Watanzania kulaani ukamataji huo kwa kuwa ni hautendi haki kisiasa.

Comments