NEC YATOA KAULI KUHUSU HATMA YA UBUNGE WA LIJUALIKA BAADA YA KUHUKUMIWA JELA
Mjadala
umeshika kasi mitaani, mitandaoni na kila mahali baada ya Mahakama ya
wilaya ya Kilombero kumhukumu kutumikia kifungo cha miezi sita jela bila
faini Mbunge Wa jimbo la Kilombero Mhe. Peter Lijualikali (30)
kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Mbunge
huyo, akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na mwenzie Stephano Mgata (35)
walitenda kosa hilo Machi 1, 2016 saa 4 asubuhi Kwenye kikao cha Baraza
la Madiwani katika eneo la Kibaoni ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya
Kilombero, mkoani Morogoro.
Imeelezwa
kuwa kwa pamoja walifanya fujo kinyume na kifungu namba 89 kifungu
kidogo cha kwanza B, cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa
marejeo mwaka 2002, ambapo washtakiwa walikana mashtaka na hivyo kufanya
kesi kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na upande wa mashtaka
ukathibitisha bila kuacha shaka.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan ameibuka
na kukata kiu ya wananchi ya kutaka kujua endapo baada ya hukumu hiyo
Mhe. Lijualikali ataendelea kuwa mbunge.
Akihojiwa
na TBC One wakati wa taarifa ya habari ya saa mbili jana usiku, Bw.
Kailima aliweka bayana kwamba mbunge huyo ataendelea na wadhifa wake kwa
kuwa sheria inasema ili kupoteza kiti ni lazima uwe umepewa adhabu ya
kifungo cha ZAIDI ya miezi sita jela.
"Ibara
ya 67(2)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza mambo
yanayotoa sifa ya kuwa Mbunge kutoka madarakani ni kifungo cha zaidi
ya miezi sita jela. Huyu bwana kafungwa miezi sita kwa hiyo bado
hajapoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge akiwa gerezani na baada ya
kumaliza kifungo chake", alisema Bw. Kailima.
Ad
Comments
Post a Comment