NIMEKUWEKEA HAPA MAMBO 19 AMBAYO MWANASHERIA MKUU WA CHADEMA TUNDULISU AMEYAZUNGUMZA KWENYE MKUTANO NA VYOMBO VYA HABARI HII LEO

 NA SHADRACK ALPHONCE

1. Kabla Mhe. Lijualikali ajawa Mbunge alikuwa diwani wa Ifakara mjini, alipata kura nyingi sana.
2.  Hii Vita ni ya siku nyingi toka mwaka 2012, kabla hajawa diwani hakuwahi kuna kesi Polisi, baada ya kuwa diwani amekuwa na kesi 6.
3. Kesi zote hizi zimekuwa na sura za kisiasa, wakati Uchaguzi wa 2015, alikuwa na kesi 3.

4. Wakati Mbunge wa Kilombero akiwa wa CCM hakukuwa na shida lakini baada Mbunge wa CHADEMA kushinda kumekuwa na shida kubwa.
5. Mhe. Lijualikali ni mfungwa wa kisiasa, amefungwa kwa sababu ya vita ya ccm na Upinzani.
6.  Mhe. Lema na Mhe. Lijualikali ni wafungwa wa kisiasa, wasifikirie kumfunga Lijualikali CCM itapendwa Kilombero wasahau.
7. Wasidhanie kumfunga Lijualikali wanamuondolewa sifa za kuwa Mbunge, Katiba ibara 67 .2 (c) inaeleza.
8.  Mara baada ya kupata taarifa, tumeanza taratibu za kukata rufaa,baada ya siku 3 tutakuwa tushakamilisha taratibu za kukata rufaa.
9. Kuhusu Lema hatuwezi kukubali wakaendelea kumnyanyasa Lema kwa sababu za kisiasa, wakipiga danadana dhamana yake.
10. Siku ya Jumamosi mimi na M/kiti Taifa ,Mhe. Mbowe tutakwenda kumtemebelea Lema gerezani na kuongea na waandishi wa habari.
11. Hata kama Mhe. Lijualikali alimpiga kweli askari, ingawa tunajua sio kweli, lakini haiwezi kumfutia sifa za kugombea Ubunge.
12. Haya masuala ya kukamata wabunge kuwasafirisha usiku zaidi ya 500km ni mambo ya ajabu,shtaka lenye dhamana lakini wanafanya siasa.
13. Kuna wajinga wanadhani kufungwa kwa Mhe. Lijualikali atapoteza ubunge wake, washauri wao wanawadanganya.
14. Wanatumia Jeshi la Polisi na watu kama wakina Lipumba katika Vita hii ya kisiasa, mambo haya yanaharibu sifa ya Nchi huko nje.
15. Lengo lilikuwa kumfunga Mhe. Lijualikali kabla ya Uchaguzi, Mhe. Lijualikali ana haki ya kuchagua M/kiti wa Halmashauri.
16. Tuna Rais wa ajabu haijawahi kutokea, mwaka 1963 tulipatwa na njaa,Nyerere hakuona aibu kusema tuna njaa.
17. Rais huyu ni wa kwanza kuwatakia Watanzania wenye njaa hatowapa chakula, Nyerere hakuona aibu kusema tuna njaa.
18. Kwa suala la Kagera na Njaa, tunapaswa kupinga haya kwa kila Mwenye akili, Rais ameenda Kagera kuwatusi Watanzania.
 19. Mlimba na Kilombero tumeshinda kote huko, mara baada ya Uchaguzi Mkuu Vita na Mhe. Lijualikali ikaanza rasmi.

Comments