OFFSIDE KUONDOLEWA KWENYE MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU
Raisi mpya wa FIFA Gianni Infantino anaonekana kutaka
kubadili soka kabisa.Infantino anaonekana kuondoa kila kitu cha Sepp
Blatter na kuleta vyake.Baada ya kuongeza timu zitakazoshiriki kombe la
dunia 2026 kufikia timu 48 sasa Infantino amekuja na mpya.Kwa kumtumia
mkurugenzi wa mambo ya ufundi wa FIFA Marco Van Basten amependekeza
baadhi ya sheria mpya katika soka.
Kuondoa offside.
Akihojiwa na gazeti la Ujerumani liitwalo Bild,Van Basten
amesema wanawaza kuondoa mchezo wa kuzidi katika soka.Alisema “sipati
picha soka isipokuwa na ofside,washambuliaji watapata nafasi nyingi sana
za kufunga”.Van Basten alisema mpira wa miguu utakuwa wakuvutia sana
kama offside itaondolewa na anaamini jambo hilo litawafurahisha
mashabiki na washambuliaji.
Kubadili upigaji wa penati.Van Basten pia anaona kuna haja
kubwa kwa FIFA kubadili aina ya upigaji wa penati. Kwa sasa adhabu ya
penati mchezaji anauweka mpira mita kadhaa karibu na goli na
kuupiga.Lakini Van Basten anaona penati ibadilishwe.Anataka mpiga penati
auweke mpira mita 25 kabla ya goli na kama anaweza atembee nao kuelekea
golini kwa muda usiozidi sekunde nane.Aina hii ya upigaji penati sio
ngeni kwani mwaka 1999 ilishafanyiwa majaribio nchini Marekani.
Kupunguza adhabu mipira ya kushika.Van Basten anaona kama
adhabu ya kadi nyekundu ni kali mno kwa tukio hilo.Na analiona kama
tukio dogo lisilohitaji kadi nyekundu na anazani inapaswa ipunguzwe
adhabu hiyo.Kusitolewe kadi nyekundu mpira ukishikwa.Adhabu kam ile ya
tukio la Luis Suarez mwaka 2010 wakicheza dhidi ya Ghana aliposhika
mpira wakati ukiingia golini Van Basten anataka kadi iwe ya njano.
Kapteni awe mtu pekee kuongea na mwamuzi.Kama katika Rugby
ni kapteni tu anayeongea na mwamuzi,asiruhusiwe mtu yeyote,mchezaji
yeyote kuongea na mwamuzi.
Style ya faulu ya mchezo wa kikapu.Katika mchezo wa kikapu
pale mchezaji anapocheza faulu tano anatakiwa atoke uwanjani.Na sasa Van
Basten anaamini staili hiyo inapaswa kuletwa katika soka.
Kupunguza idadi ya mechi.Hii itafurahiwa sana na makocha
wageni Uingereza.Alianza Van Gaal akaja Jurgen Klopp walilalamikia idadi
ya mechi kuwa nyingi Epl.Van Basten anataka idadi ya mechi zipunguzwe
kutoka mechi 80 kwa msimu hadi 50 kwa msimu.
Kuongeza idadi ya Substitution.Van Basten anatamani
kuongeza idadi ya wachezaji wa sub kuanzia 5-7,kwa muda mrefu wadau wa
soka wamekuwa wakizungumzia kuhusu suala la kuongeza wachezaji wa akiba
na sasa FIFA inatarajia kuliangalia suala hili.
Kuzifanya dakika 10 za mwisho kutumika ipasavyo.”Tunajua
kutokana na kuongeza idadi ya wachezaji wa akiba pamoja na aina ya
upigaji penati vitachukua mda mrefu uwanjani na itatubidi kuhakikisha
dakika 10 za mwisho zinatumika kiuhakika” Van Basten alisema
watahakikisha hakuna upotezaji muda katika dakika zamwisho za mchezo.
Hayo ni mapendekezo tu kutoka kwa mkurugenzi wa ufundi wa
FIFA.Na sasa atawasilisha mapendekezo hayo katika kamati ya FIFA yaweze
kujadiliwa.
Comments
Post a Comment