PAYET AGOMA KUFANYA MAZOEZI AKITA KUONDOKA KLABUNI HAPO
Mkufunzi wa klabu ya West Ham Slaven
Bilic amesema kuwa mshambuliaji Dimitri Payet hataki tena kuichezea
West Ham , lakini klabu hiyo haiko tayari kumuuza.
Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akihusishwa na swala la kuihama timu hiyo.
''Tumesema kuwa hatuwezi kuwauza wachezaji wetu wazuri lakini Payet hataki kutuchezea tena'', alisema Bilic.
''Hatuwezi kumuuza''. Payet alijiunga na West Ham kutoka Merseille kwa kitita cha pauni milioni 10.7 mnamo mwezi Juni 2015.
Alifanikiwa
katika msimu wa kwanza na klabu hiyo ,akifunga mabao 12 na kuteuliwa
miongoni mwa uzo la wachezaji bora la kila mwaka.
Ijapokuwa amefunga mara tano msimu huu, Payet
ameshindwa kufikia kiwango kama hicho na gazeti la The Sun liliripoti
wiki ilioipita kwamba Bilic alimuagiza mchezaji huyo kubadili tabia
yake.
Aliwachwa nje katika mechi ya FA siku ya Ijumaa ambapo West Ham ililazwa 5-0 na Manchester City.
West
Ham iko nafasi ya 13 katika ligi ya Uingereza, alama saba juu ya eneo
la kushushwa daraja na sasa itakwaruzana na Crystal Palace siku ya
Jumamosi.
Comments
Post a Comment