RUFAA YA POLISI DAR DHIDI YA SIMBA YATUPILIWA MBALI


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetupilia mbali rufani ya klabu ya Polisi Dar dhidi ya Simba katika kombe la FA kwa madai kwamba haikuambatana na ada ya rufaa.
Polisi ilikata rufaa kwa madai kwamba Simba ilimjumuisha beki Novatus Lufunga katika kikosi chake wakati akiwa bado anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyeonyeshwa katika mechi ya mwisho ya mashindano hayo msimu uliopita.

Comments