RUSHWA YAMUWEKA LUMANDE KATIBU WA BARAZA LA KATA


Image result for rushwa


KATIBU wa Baraza la Kata ya Itumba, wilayani Igunga, mkoani Tabora, Iddi Mohamed(46) amefikishwa katika Mahakama ya wilaya kwa tuhuma ya kuomba rushwa ya Sh
100,000.
Akimsomea mashitaka mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Igunga, Ajali Miranzi, mwendesha mashitaka wa Takukuru wa wilayani Nzega, Aidani Samali, alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 6, mwaka 2016.
Inadaiwa kuwa, Mohamed aliomba rushwa ya Sh 100,000 kutoka kwa Kusonga Ludula aliyekuwa na kesi ya madai ya mashamba katika baraza hilo la kata ili amsaidie kesi yake kupata ushindi.
Mwendesha mashitaka aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nambari 11 ya mwaka 2007.
Hata hivyo mshitakiwa alikana mashitaka na yuko nje kwa dhamana ya Sh milioni moja na kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 19 mwaka huu itakapotajwa ten

Comments