SERIKALI YATANGAZA KULETA PEDI ZINAZOWEZA KUTUMIKA ZAIDI YA MARA MOJA
Alisema hayo jana katika mahojianio na EATV kuhusu jitihada za
serikali za kuhakikisha afya ya watoto wa kike inalindwa na kuepusha
utoro mashuleni
kutokana na tatizo la hedhi isiyo salama hasa maeneo ya
vijijini na wale wasio na uwezo wa kuzipata taulo hizo.
“Sasa hivi tupo kwenye mchakato wa kuangalia zile pedi ambazo vijana
wanaweza kutumia mwenzi mmoja, miwili hata mwaka mzima, hata kwa miaka
miwili,” alisema Kigwangalla. “Kuna nchi mbalimbali wameingiza kwenye
soko bidhaa na namna hiyo kwa hiyo na sisi tunaendelea kuangalia tafiti
mbalimbali kuhusu usalama wa hizi pedi ambazo unaweza kuzitumia kwa muda
mrefu,”
Aliongeza, “Kwa hiyo tunaangalia kama na sisi tunaweza kuziruhusu
kuingia nchini na sisi tuziingize sokoni. Lengo letu ni kuangalia
usalama kwanza kabla hatujaziruhusu kutumika,”
Amesema serikali inahimiza wazazi na walezi wa watoto wa kike
wanapoona mabadiliko yametokea kwa mabinti zao wawafundishe namna ya
kujitunza kwa kutumia vifaa ambavyo vipo na vinapatikana kwa urahisi
sambamba na kuwapa elimu zaidi ili wawe wasafi na kujiepusha na magonjwa
yakuambukizwa.
Kwa upande wake mbunifu wa taulo za kike ambazo zinaweza kutumika
zaidi ya mara moja Bi.Jennifer Shigoli amesema katika maeneo mbalimbali
waliopitia kwa ajili ya kubaini changamoto zinazowakuta watoto wa kike
katika kipindi cha hedhi wamebaini ukosefu wa elimu ambayo baadhi ya
watu wamepata magonjwa yatokanayo na hedhi isiyo salama hivyo ameiomba
serikali kutoa ushirikiano katika kumaliza tatizo hilo nchini.
Comments
Post a Comment